KWA UFUPI
- Alisema kuwa NMB itakuwa ikitoa Sh32 milioni kwa mwezi kwa ajili ya kusaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati vikiwamo viwanda vidogo vya usindikaji mazao, huduma na wazalishaji mali na mara nyingi mikopo hiyo huwa chini ya mwaka mmoja.
Dar es Salaam. Benki ya NMB imetiliana saini mkataba wa Sh 147bil na European Investment Bank (EIB) kwa ajili ya kusaidia wajasiriamali wadogo nchini
Katika makubaliano hayo na EIB, NMB itakuwa ikisaidia kutoa mitaji ya vianzio kwa biashara na uwekezaji kwa wajasiriamali hao wa Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali cha NMB, Filbert Mponzi, alisema: “NMB imetoa mikopo nafuu kwa vikundi vya wajasiriamali zaidi ya 45,000 nchini, na vikundi vya kati zaidi 10,000 kupitia matawi yake 150.
Alisema kuwa NMB itakuwa ikitoa Sh32 milioni kwa mwezi kwa ajili ya kusaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati vikiwamo viwanda vidogo vya usindikaji mazao, huduma na wazalishaji mali na mara nyingi mikopo hiyo huwa chini ya mwaka mmoja.
Naye Ofisa wa Fedha wa NMB, Waziri Barnabas alisema: “NMB tayari pamoja na kwamba benki ina uwezo kifedha kusaidia sekta mbalimbali, lakini kwa kuongezewa nguvu na EIB itatusaidia kuwafikia watu wengi zaidi kuwawezesha mitaji.”
No comments:
Post a Comment