Uchumi na Biashara
WAKULIMA wa vitunguu mkoani Singida msimu uliopita walizalisha tani 17,334 za vitunguu zenye thamani ya sh.bilioni 3.5 katika maeneo yanayolima zao hilo kwa wingi na kuuzwa kwa wafanyabiashara kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi.
Taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisa Kilimo Mkoa wa Singida, Bw.Deusdedit Rugangila zilieleza kuwa
wafanyabiashara kutoka Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, India na Comoro na wengine kutoka Mikoa ya Manyara, Arusha, Morogoro, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza ndiyo wanaoongoza kununua vitunguu vya Singida kwa wingi katika soko lililotengwa.
Bw. Rugangila aliyataja, maeneo yanayolima vitunguu kwa wingi Wilaya ya Iramba kuwa ni Mwanga, Nduguti, Gumanga, Ilunda na maeneo mengine ni Iguguno, Ulemo, Msingi, Singa.Maeneo yanayolima vitunguu wilayani Singida ni Mtinko, Merya, Kinyeto, Ilongero, Ikhanoda na mengine ni Mdida, Mwanyonye, Msange na Ngamu.
Ilieleza wakulima wa vitunguu huanza kutayarisha mashamba yao mwezi Novemba hadi mwezi Aprili, tayari vitunguu huanza kuvunwa na kuuzwa
Bw. Rugangila alitaja mbegu za vitunguu zinazolimwa sana Singida kuwa ni Red Bombay, Red Globe, Red Creole na Tropicana na amewahimiza wakulima kutumia mbegu bora ili waweze kupata mazao mengi na bei nzuri ili kukidhi mahitaji ya soko.
Hata hivyo amewahimiza wakulima kutumia mashamba darasa yaliyopo kwenye maeneo yao ili waweze kufikia malengo yanayotakiwa.
Mkoa wa Singida katika miaka ya nyuma ulikuwa maarufu sana kwa uzalishaji wa vitunguu lakini sasa uzalishaji wake umeanza kupungua kutokana na uhaba wa mvua,kukosa dawa za kuua wadudu, ukungu na utaalamu mdogo juu ya upandaji, uvunaji na utunzaji wake.
Amana yazindua huduma zake Dar
Makumba Mwenezi na Mariam Bokero
WATANZANIA wameanza kunufaika na huduma za kibenki zinazofuata misingi ya dini ya Kiislamu baada ya kuzinduliwa rasmi kwa benki ya 'Amana'ambayo itaendeshwa kwa kufuata misingi ya sharia na maelekezo ya ufanyaji biashara ndani ya Quran tukufu.
Benki hiyo ambayo ni benki ya kwanza ya Kiislamu Tanzania ilizinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na kuanza kutoa huduma siku hiyo hiyo, huku ikiwa tayari imetoa ajira kwa zaidi ya Watanzania 50 katika nafasi mbalimbali.
Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa benki hiyo, Mwenyekiti wa bodi, Bw. Haroon Pirmohamed alisema Amana benki itatoa huduma na bidhaa ambazo zitafuata misingi ya sharia na ambazo zimepitiwa na Bodi ya Sharia kwa mujibu wa Quran.
Alisema huduma hizo ni pamoja na akaunti za biashara zisizokuwa na riba yoyote, akaunti za akiba, akaunti maalumu za wanawake na watoto, akaunti za hijja na akaunti za akiba kwa ajili ya nyumba za ibada zilizosajiliwa yaani Ihsan akaunti.
Bw. Permohamed alisema benki imedhamiria kutoa huduma katika mazingira rafiki kwa wateja hasa wale wote wasiofurahishwa na huduma za riba zinazotolewa na benki nyingine na kudai kuwa huduma za benki hiyo ni kwaajili ya watu wote wakiwemo Waislamu na wasiokuwa Waislamu.
Amana benki inatokana na michango ya mjumuiko wa wafanyabiashara wanao amini na kufuata misingi ya sharia kikamilifu na inamilikiwa na Watanzania wazalendo wakimiliki hisa tofauti huku benki ikiwa na kiasi cha mtaji wa sh. bilioni 21.1 mpaka sasa......chanzo-majira

No comments:
Post a Comment