- Mtafiti maarufu ndani na nje ya nchi katika masuala ya utafiti na magonjwa ya kilimo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Mikocheni, Dk Joseph Nduguru, anasema kuwa teknolojia ya Uhandisi Jeni ina lengo la kuongeza mavuno kwa mkulima
- Katika kitabu chake kiitwacho Starved for Science, How Biotechnology is being kept out of Africa, mwandishi Robert Paarlberg anaeleza sababu za wakulima wengi barani Afrika kuwa maskini kwa kuwa tu wameipuuzia teknolojia ya Uhandisi Jeni au kwa Kiingereza Genetically Modified Organism (GMO)Kwa hali ilivyo nchini, wakulima wamekuwa wakipotoshwa kuhusu ukweli wa teknolojia hii. Hii inatokana na wananchi wengi kusikiliza hoja za upande mmoja ambazo hazina uthibitisho wa kitafiti wala kisayansi kuhusu faida za teknolojia hiyo. Wanachopotoshwa ni kuwa teknolojia hiyo ina madhara kwa afya ya binadamu.Wananchi wasipoelimishwa maana na umuhimu wa teknolojia hii, inawezekana nchi yetu ikachelewa kwa kiasi kikubwa kufanya mapinduzi ya viwanda kupitia tafiti, sayansi na teknolojia katika kilimo chetu.Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia majukwaa mbalimbali, yakiwemo Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo Tanzania (OFAB) pamoja na wadau mbali mbali wa kilimo, wamekuwa wakifanya jitihada kuelimisha wananchi kuhusiana na faida za kutumia teknolojia ya uhandisi Jeni.Kauli za wataalamuMtafiti maarufu ndani na nje ya nchi katika masuala ya utafiti na magonjwa ya kilimo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Mikocheni, Dk Joseph Ndunguru, anasema kuwa teknolojia ya Uhandisi Jeni ina lengo la kuongeza mavuno kwa mkulima.Kinachofanyika katika teknolojia hiyo, anasema ni kutengeneza kinga kwa mmea au mifugo ili isipate mashambulizi ya magonjwa mbalimbali.“Kinachofanyika kwenye teknolojia ya Uhandisi Jeni hakina tofauti sana na teknolojia inayotumika wakati wa kutengeneza dawa ya Insulini kwa ajili ya wagonjwa wa Kisukari” anaeleza.Dr Ndunguru anatoa mfano wa ugonjwa wa mihogo ujulikanao kwa jina la Bato Bato, ambao ameufanyia utafiti kwa kipindi kirefu.Anasema ugonjwa huo unasababishwa na aina fulani ya kirusi aitwaye cassava mosaic virus anayeshambulia majani ya muhogo kupitia inzi wadogo weupe.Kuhusu teknolojia ya Uhandisi Jeni inavyofanya kazi katika zao la muhogo, anasema kuwa kinachofanyika ni kuchukua mbegu na kuipandikizia aina ile ile ya kirusi ambayo huathiri muhogo.Baada ya mchakato huo muhogo uliopandikiziwa ile DNA (Vinasaba) ya kile kirusi huwa na kinga na haiwezi tena kushambuliwa na aina ile ya kirusi. Kwa maneno mengine muhogo ule uliofanyiwa Uhandisi Jeni huwa imara kukabiliana na ugonjwa wa Bato Bato.Teknolojia ya Uhandisi Jeni iliyofanyiwa majaribio mengi katika Taasisi ya Kilimo ya Mikocheni ikihusisha wataalamu wengi kutoka mataifa makubwa duniani, imethibitisha kuwa mimea yote inayotokana na teknolojia hii haina madhara kwa binadamu.Kwa kutojua manufaa ya teknolojia hii, mkulima wa mihogo kutoka Bagamoyo, Juma Shaban, hajui nini afanye katika mazao yake ambayo yameshambuliwa kwa kiasi kikubwa na aina hiyo ya kirusi.Yeye anaamini kwamba majani ya mihogo yake yamekauka kutokana na ukame, na ndiyo maana hupata mavuno kidogo ya mihogo.Asichokijua ni kuwa shina la muhogo lililoathiriwa na virusi vya ugonjwa huo, likikatwa na kupandwa sehemu nyingine bado hali ya ugonjwa itaendelea kuwepo na kuambukiza eneo hilo pia.Kwa mujibu wa Dk Ndunguru, virusi vinavyosababisha magonjwa ya mimea kama muhogo (cassava mosaic virus) havina madhara kwa binadamu, na ndiyo maana kisamvu cha muhogo ulioathiriwa na ugonjwa wa Bato bato bado kinaweza kuliwa , japo watu wengi hawajui.Naye Profesa Calistius Juma kutoka Chuo Kikuu cha Harvard Marekani, anasema kupitia tafiti zake teknolojia hiyo haina madhara na imeonyesha mafanikio katika nchi za Afrika Kusini, Burkinafaso, Misri na Sudan.Tafiti zake zinaweka bayana ukweli kuwa teknolojia hiyo, ina nafasi kubwa ya kuleta mafanikio ya kilimo hasa katika maeneo ya ardhi zisizokuwa na rutuba. Mfano mzuri ni India inayozalisha kwa kiwango kikubwa zao la Pamba, licha ya ukweli kuwa ardhi ya nchi hiyo haina rutuba ya kutosha.Kwa nini inapigwa vita?Watu wamekuwa wakijiuliza kwa nini teknolojia hii inapigwa vita na baadhi ya watu na hata taasisi mbalimbali? Jibu ni rahisi, mbegu za mazao zilizofanyiwa Uhandisi Jeni zina kinga ambayo hustahimili magonjwa, hivyo mkulima anaweza asitumie kabisa mbolea.Kwa sababu hiyo, tukiruhusu sheria zetu kukubali moja kwa moja Uhandisi Jeni, kuna baadhi ya viwanda vitakosa soko la mbolea wanazozalisha.source,mw'nchi
Tuesday, September 3, 2013
Teknolojia yenye manufaa kwa wakulima nchini,yagundulika..!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment