Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, September 14, 2013

Mbilimbi hutumika kufanyia mazoezi ya kubeba dawa za kulevya Jijini D’Salaam....!!!


Kulingana na utafiti uliofanywa na chanzo chetu, hii katika vijiwe, baadhi ya vijana wamebuni utamaduni wa kufanya mazoezi ya kubeba dawa za kulevya tumboni kwa kumeza mbilimbi bila kutafuna, ili iwapo itatokea nafasi ya aina hiyo muda wowote, wawe tayari kuingia kazini. Uchunguzi uliofanywa maeneo ya Kinondoni, Magomeni, Vingunguti, Manzese, Msasani, na Temeke, umegundua zao la mbilimbi limekuwa likitumika kama kifaa cha kupima uwezo wa mbebaji wa dawa za kulevya.

Katika tukio lililofanyika hivi karibuni, raia wa Canada, Tabitha Leah Ritchie (28) amekamatwa nchini Colombia baada ya kujaribu kupanda ndege kurejea Canada akiwa na tumbo bandia la ujauzito alimokuwa ameficha dawa ya kulevya aina ya Cocaine.
Ni wazi kwamba vita vya kupambana na dawa za kulevya si ndogo, kwani kwa namna inavyoonekana ni kwamba wenye kujihusisha na biashara hiyo, licha ya baadhi kudaiwa kushirikiana na wafanyakazi wasio waaminifu katika vyombo vya ulinzi, wanabuni mbinu tofauti kukwepa mkono wa sheria.
Tatizo la dawa za kulevya ni la dunia nzima, sio Tanzania au Afrika tu, kuna raia wengi wa kigeni wamenaswa nchini Colombia mwaka huu wakiwa na dawa za kulevya.

mw'chi

No comments:

Post a Comment