
Somalia imeshuhudia maendeleo si haba tangu Al Shabaab kufurushwa mjini Mogadishu.
Muungano wa Ulaya kwa ushirikiano na serikali ya Somalia, hii leo umeandaa kongamano la kimataifa mjini Brussels kutathmini hali inavyoendelea nchini Somalia
Wanadiplomasia wanasema wanatarajia kuwa wahisani wataahidi kuchangisha mamilioni ya dola kama msaada kwa Somalia kwenye mkutano huo.
Mkutano huo unawaleta pamoja maafisa wa serikali , mashirika ya misaada na taasisi za kifedha.
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, aliambia BBC kuwa mkataba mpya unaopendekezwa na ambao unaipa nchi hiyo usemi mkubwa kuhusu mahitaji yake ya maendeleo, utaifaidi nchi ya Somalia pakubwa sana.
Duru zinasema kuwa matatizo chungu nzima yangali yanaikumba Somalia ikiwemo serikali kudhibiti sehemu ndogo tu ya nchi na ripoti za utumizi mbaya wa pesa.
BBC
No comments:
Post a Comment