Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, September 5, 2013

Matunda ni tiba kwako sio Anasa,... Magonjwa na Tiba kupitia Matunda!!




  • Hizi ni baadhi ya faida za kula matunda na zenye kuonyesha umuhimu na kuwavutia wengi kuyatumia kila siku.

Kwa jumla imezungumzwa au kuandikwa mara nyingi kuhusu umuhimu wa kula matunda ikiwezekana kabla ya kila mlo, lakini hiyo hainifanyi nishindwe kukumbusha kuhusu hilo.

Kinachonifanya nilizungumzie hili ni kutokana na baadhi yetu kudharau kula matunda katika milo yetu bila kujua faida au madhara yake.
Zipo faida nyingi za kula matunda ukiachilia mbali ladha yake. Pia yana virutubisho vingi , vitamini za aina mbalimbali ambazo hupatikana kwenye matunda. Matunda pia husaidia kupunguza matatizo ya moyo, kiharusi, shinikizo la damu, lehemu, aina mbalimbali za saratani, matatizo ya uwezo wa macho kuona na mengine mengi.
Faida za matunda kama ndizi, parachichi, embe, zabibu, nanasi, chungwa na papai ni nyingi pengine kuliko madhara mengi kwenye miili yetu.
Kwa mfano, wataalamu wanaeleza kuwa embe ni chanzo cha vitamini A na E. Vitamini A husaidia kuboresha macho kwa kukuwezesha uone vizuri.
Pia, husaidia kupunguza uwezekano wa upofu kwa wazee kwa kuimarisha macho yao.
Parachichi lina vitamini E ambayo faida yake ni kupunguza kiwango cha lehemu mwilini, hivyo hufanya moyo kuwa na afya njema.
Ndizi ina vitamini B6 na madini ya potassium, ndizi zina madini mengi ya potassium ukilinganisha na matunda mengine ambayo husaidia kupunguza ongezeko la shinikizo la damu.
Chungwa ni moja ya matunda muhimu pia kwa kuwa lina vitamini C na madini ya potassium, vitamini iitwayo ‘folate’’ (B-Group Vitamin ) ambayo husaidia katika kujengeka kwa ubongo wa mtoto, kwa mama mjamzito.
Pia, chungwa lina kemikali zijulikanazo kama ‘hesperidin’, ambazo hupunguza kiwango cha lehemu kwenye damu. Papai ni tunda lenye vitamini A na C, lina kimeng’enyo kijulikanacho kama ‘papain’ ambayo husaidia katika kusaga au mmeng’eo wa chakula, pia husaidia kuboresha afya ya ngozi. Nanasi ina kimeng’enyo asilia ‘bromelain’’ ambacho husaidia kuvunjavunja protini, hivyo husaidia katika mmeng’enyo wa chakula.
Vilevile, bromelain husaidia kupunguza ukuaji wa seli za saratani na kuchochea uponaji wa vidonda kwa haraka.
Zabibu ni moja ya matunda yenye faida kwa kuwa ina madini ya manganese, ambayo hupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya moyo kwa kusaidia kushusha kiwango cha shinikizo la damu.
Hizi ni baadhi ya faida za kula matunda na zenye kuonyesha umuhimu na kuwavutia wengi kuyatumia kila siku.
Nchini Tanzania sasa kuna ugonjwa umeshika kasi , yaani wa ‘Bone and Curtilage Erasion’. Kwa tafsiri rahisi ni kusagika kwa mifupa. Ugonjwa huu siku za nyuma kidogo haukuwa ukiwasumbua wengi kama ilivyo sasa.
Licha ya kuwa na maumivu makali, tiba yake anayo mgonjwa mwenyewe ambayo ni kufanya mazoezi na kula matunda kwa wingi kwani husababishwa na ukosefu wa kula vyakula vyenye vitamini, ambapo kwa maisha ya kawaida ni maharage, njegere, na mboga za majani siyo chakula kipya kwani ndiyo tunavila karibu kila siku, lakini matunda ni suala ambalo watu hulichukulia kama anasa wakati ni moja ya tiba kuu mwilini.
Wengi wa wagonjwa wa ugonjwa huu wamekuwa wakishauriwa kula matunda. Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani wengi wetu tunadharau kula matunda licha ya kuwa na faida kubwa mwilini, ikiwamo kutibu au kuzuia baadhi ya magonjwa.

No comments:

Post a Comment