
Serikali ya Kenya, imesema nchi hiyo ipo katika vita na wapiganaji wa jihadi kutoka nchini Somalia Al Shabaab.Pia Serikali nchini humo imekanusha taarifa zinazodai k uwe p o kwa s h amb u l i o linalodaiwa kufanywa na Al Shabaab katika jengo la kibiashara la Westgate, Septemba 21 mwaka huu, zilipuuzwa
. Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), watu 67 walipoteza maisha katika shambulio hilo ambalo lilidumu kwa siku nne ndani ya jengo hilo.Juzi usiku, Wakenya na raia wa nchi nyingine waliopoteza ndugu zao katika shambulio hilo, waliwasha mishumaa nje ya jengo hilo ili kuwakumbuka waliokufa. Magazeti ya Kenya yalidai Idara ya Usalama nchini humo ilitoa ilani mwaka mmoja uliopita juu ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Al Shabaab, kupanga kufanya mashambulizi Mjini Nairobi na Mombasa.