Tanga. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeanza kugawa mashine
za kisasa za kufyatulia matofali katika halmashauri za mkoani Tanga,
huku likiwataka vijana kuzitumia kama sehemu ya ajira yao.
Meneja wa NHC mkoani Tanga, Issaya Mshamba
aliyasema hayo juzi mjini Muheza alipokuwa akikakabidhi mashine hizo kwa
mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, Ibrahim Matobu.
“Shirika la Nyumba limeamua kuwakumbuka vijana kwa
kuwaletea mashine hizi ili waweze kujiajiri kupitia vikundi
vitakavyosimamiwa na halmashauri zao, kwa hiyo ni vyema wazitumie kwa
manufaa yao na Taifa kwa jumla,” alisema Mshamba.
Alisema NHC imetoa mashine 40 zitakazogawiwa katika halmashauri 10 na inatarajia kuwa vijana ndiyo watakuwa wa kwanza kunufaika.
Akizungumza baada ya kupokea mashine hizo, Matovu
alisema kila kikundi kitakachokabidhiwa mashine, atakitafutia zabuni ya
kusambaza matofali.
No comments:
Post a Comment