Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, November 9, 2013

JOB:Part Time IT Administrator

Part Time IT Administrator
Canadian Cooperation Office,

Date Listed: Nov 7, 2013
Phone: No Phone Calls
Area: Dar Es Salaam
Application Deadline: Nov 15, 2013

Position Description:
From The Guardian November 7, 2013
The Canadian Cooperation office is seeking a Part time IT Administrator.
The successful applicant will have a university degree in Information technology or related field with a minimum of 2 years professional experience in hardware and software maintenance.
The successful candidate must bea team player who is highly motivated; flexible; dynamic and has strong organizational capabilities. Applicant must have competency with Microsoft and other commonly used computer software applications. Also must have full written and oral fluency in English and Swahili. The position will be part-time with the commitment of 2-3 hours twice a week and be on call for the remaining time for the period of one-year contract. The position is currently vacant and available for an immediate start.


Application Instructions:
Interested candidate please write to hr@ccotz.org  or services@ccotz.org  to request for application instructions. Deadline for the receipt of applications will be November 15th, 2013 at 12:00 noon.

Tuesday, October 29, 2013

NAFASI MPYA ZA KAZI BENKI KUU YA TANZANIA,MWISHO 11st NOV 2013

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES


The Bank of Tanzania, an equal opportunity employer and Tanzania’s central bank, is looking for suitably qualified young Tanzanian citizens of high personal integrity to fill the following vacant positions at the Head Office and at its Branches in Mwanza, Mbeya, Arusha, Zanzibar and Training Institute, Mwanza.

1.Position: Accountant III (Domestic Payments and Settlement) - 2 Posts
Reports to: Head of Division
Contract type: Contract for unspecified period of time
Location: Head Office, Dar es Salaam
Job Purpose:
To execute accounting duties relating to domestic payments and settlement, reconciliation, accounting entries and examination of payments.
Primary Duties and Responsibilities:
a) Preparing, examining and analyzing periodic statements of financial position and statement of comprehensive income to assess accuracy, completeness and conformance to reporting standards;
b) Monitoring and reviewing accounting entries and related system reports for accuracy and completeness;
c) Resolving accounting entries discrepancies;
d) Reviewing and recommending International Financial Reporting Standards (IFRS) which are relevant to the Bank;
e) Reconciling internal and intermediary accounts;
f) Maintaining accounting records and preparing accounts and management information;
g) Providing advice and support to internal and external auditors in completing audits;
h) Examining and verifying payments;
i) Performing other related duties as may be assigned by the Head of Division.
Education/Professional Qualifications Required:
a) Bachelor‘s Degree in Accounting or its equivalent from an accredited institution;
b) Master’s Degree will be an added advantage.

Tuesday, October 15, 2013

Watoto milioni mbili na nusu hawako shuleni Tanzania


Tafiti zinaonyesha sababu za wanafunzi kutokuwapo shuleni ni pamoja na utoro, mimba za utotoni, umaskini na mwamko mdogo wa wazazi kuhusu elimu.
Wakati ripoti ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 , ikionyesha kuwa asilimia 44 ya Watanzania wote ni watoto chini ya umri  wa miaka 15, watoto milioni mbili na nusu  wamebainika kukosa fursa ya kupata elimu ya msingi.
Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu, anasema kuwa sababu kubwa ya watoto wengi kutokuwapo shuleni licha ya kuwa na umri wa kwenda shule  ni utoro.
“Hata ukiangalia BEST (Kitabu cha Takwimu za Elimu ya Msingi) ya mwaka 2012 utaona kuwa utoro ulikuwa sababu kubwa ya watoto kutokuwa shuleni,” anasema.

Kanuni bora za usalama wa kompyuta yako


Ingawa mara nyingi husemwa kuwa hakuna usalama wa asilimia mia moja kwenye ulimwengu wa teknolojia ya kompyuta, ila kinga ni bora kuliko tiba.
Umewahi kujiuliza kwa nini watu wengi wanatumia kiasi kikubwa cha fedha kuimarisha ulinzi katika maeneo yao ya makazi?
Ndivyo ilivyo, tembelea hata katika makazi ya watu wa kawaida, madirisha yamejaa nondo, nyumba zimezungukwa na kuta ndefundefu. Wengine wamefikia hatua ya kufuga mbwa kwa ajili ya kuwalinda.
Nimeanza kwa kutoa mifano hii kuonyesha umuhimu wa kuzilinda kompyuta zetu. Ingawa mara nyingi husikika ikisemwa kuwa hakuna usalama wa asilimia mia moja kwenye ulimwengu wa teknolojia ya kompyuta, ila kinga ni bora kuliko tiba.

Sunday, October 13, 2013

Serikali yatangaza nafasi za kazi 1,100

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza nafasi za kazi 1,134 katika sekta mbalimbali za ofisi za umma.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ya www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.
Katibu alifafanua kuwa nafasi 949 ni kwa ajili ya waajiri walioainishwa katika ofisi za wizara, halmashauri na nyingine 185 ni za taasisi na wakala mbalimbali za Serikali.

Friday, October 11, 2013

AFYA:Epuka chumvi za kuongeza mezani kiafya

Chumvi imepewa majina mengi kulingana na jamii ambayo mengine yanachekesha
Kila Jumapili ya mwisho ya mwezi Septemba kila mwaka huitwa Siku ya Moyo Duniani.
Lengo la siku hiyo ni  kuwapa ufahamu watu kuhusu magonjwa ya moyo ambayo ndiyo kwa kiasi kikubwa  husababisha vifo kwa wingi duniani. Tukio hili hulenga pia katika kuhamasisha njia za kujikinga na zinazoweza  kusaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa hayo.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa mwaka 2005 peke yake palitokea vifo vya watu milioni 17.2 duniani kwa magonjwa ya moyo.
Hii ni  asilimia 30 ya vifo vyote duniani huku kina mama wakiongoza kwa kufa zaidi. Pia, kila mwaka katika vizazi hai 1,000, watoto wanane huzaliwa na matatizo ya moyo katika Tanzania. Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya asilimia 20-30 ya watu wanaugua magonjwa ya moyo.

Monday, October 7, 2013

Algerian independent trade union rights are curbed

Independent trade unions and workers in Algeria are coming up against labour restrictions, in contrast to the rights enjoyed by their state-run counterparts
Algerian policemen try to take away a banner from anti-government protesters during a demonstration in Algiers (Photo: Reuters)

Independent trade unionists and workers in Algeria are facing obstacles hampering their legal rights, a Human Rights Watch report said Sunday protest organised by the Contractual Workers Union was violently dispersed, with 20 workers arrested and released on the same day.

Monday, September 30, 2013

KENYA YAINGIA VITANI...!!!


 
  Serikali ya Kenya, imesema nchi hiyo ipo katika vita na wapiganaji wa jihadi kutoka nchini Somalia Al Shabaab.Pia Serikali nchini humo imekanusha taarifa zinazodai k uwe p o kwa s h amb u l i o linalodaiwa kufanywa na Al Shabaab katika jengo la kibiashara la Westgate, Septemba 21 mwaka huu, zilipuuzwa

. Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), watu 67 walipoteza maisha katika shambulio hilo ambalo lilidumu kwa siku nne ndani ya jengo hilo.Juzi usiku, Wakenya na raia wa nchi nyingine waliopoteza ndugu zao katika shambulio hilo, waliwasha mishumaa nje ya jengo hilo ili kuwakumbuka waliokufa.   Magazeti ya Kenya yalidai Idara ya Usalama nchini humo ilitoa ilani mwaka mmoja uliopita juu ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Al Shabaab, kupanga kufanya mashambulizi Mjini Nairobi na Mombasa. 

Sunday, September 29, 2013

MAJAMBAZI WAVAMIA BENK JIJINI DAR ES SALAAM NA KUPORA ZAIDI YA MILIONI 150..


Majambazi saba akiwemo mmoja ambaye amevalia sare za polisi wameiteka benki ya I&M  jijini Dar es Salaam na kuchukuwa fedha zinazohisiwa  kuwa  ni zaidi ya shilingi milioni 150 na kutokemea kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea katika benki hiyo iliyoopo katika makutano ya mtaa wa Indira Gandi na Mosque ambapo baadhi ya mashuhuda wameelezea tukio hilo lilivyokuwa.

Saturday, September 28, 2013

Tume ya Warioba yatishia kujiuzulu....!!!

Mzee Joseph Butiku na Profesa  Mwesiga Baregu
TUME ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba, sasa inasuburi uamuzi wa mwisho wa serikali kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa hivi karibuni bungeni, ili hatimaye kwa pamoja wajumbe wa tume hiyo waamue kujiuzulu ama waendelee na majukumu yao, Raia Mwema limeelezwa.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu mbalimbali vya habari ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, katika kikao chake cha mwanzoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, sehemu kubwa ya wajumbe walikuja juu wakionyesha kukerwa na namna mabaraza ya katiba yalivyoingiliwa na Chama cha Mapinduzi.

Mali ya bilioni tisa yauzwa kwa milioni 243/-

Makao Makuu Consolidated Holding Corporation (CHC)
UTATA umegubika uuzwaji wa iliyokuwa bohari ya serikali ya Chang’ombe, Dar es Salaam inayokadiriwa kuwa na thamani ya Sh bilioni tisa lakini ikiwa imeuzwa kwa thamani ya Sh milioni 243 tu, Raia Mwema, limebaini.
Hata hivyo, wakati nyaraka za gazeti hili zikionyesha mauzo ya Sh. milioni 243, mrithi wa PSRC iliyokuwa ikisimamia mali hizo na nyingine za serikali chini ya mchakato wa ubinafsishaji, Consolidated Holding Corporation (CHC) taarifa zake rasmi zinaeleza bohari hiyo imeuzwa kwa Sh. milioni 195.9.

KUFUNGIWA KWA MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA KWA MUDA ......

...






Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba, 2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.

Friday, September 27, 2013

MUHIMU:Jifunze mpangilio wa Chakula kwa wanamazoezi..!!

 Mazoezi yana umuhimu mkubwa kwa maisha yako endapo utaweza kuyafanya kwa jinsi ipasavyo
Kujua muda wa kula na kitu cha kula kunaweza kukusaidia kupata matokeo tofauti katika ufanyaji wako wa mazoezi.
Wanasayansi wanasema kuwa ulaji na mazoezi ni vitu vinavyoenda bega kwa bega. Ni vizuri kuelewa chakula unachokula kinaathiri vipi mazoezi yako.

Warioba: Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ina upungufu..!!!


Dar es Salaam. Wakati wananchi wa kada mbalimbali wakishinikiza Rais Jakaya Kikwete kutokusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013, kwa maelezo kuwa una kasoro, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye amesema sheria ina upungufu.
Warioba alisema jana kwamba ni jambo la kushangaza sheria hiyo kueleza kuwa tume hiyo itavunjwa baada ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumu la Katiba, wakati huohuo ikieleza kuwa itahusika tena kusimamia utoaji wa elimu ya kura ya maoni.

Wednesday, September 25, 2013

Mwanamke aliyeongoza shambulizi la kigaidi la Westgate adaiwa kuuawa


Dar es Salaam/Nairobi. Huku mapambano yakiwa yamepamba moto, anayedaiwa kuwa Kiongozi wa kundi la magaidi lililovamia jengo la kibiashara la Westgate, Samantha Lewthwaite inadhaniwa kuwa ameuawa.
Lewthwaite, ambaye anaitwa kwa jina la utani la ‘Mjane Mweupe’ anadaiwa kuongoza shambulizi hilo lililosababisha vifo vya watu 62 na kujeruhi wengine 170 mjini Nairobi.

Wanawake wawili wakamatwa na maiti yenye madawa tumboni!!!


Wanawake wawili Nasra Omari (36) na Mwanaisha Kapama (36), ambao ni wakazi wa Kigogo Luhanga, jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na maiti iliyokuwa na dawa za kulevya (aina ya heroin pipi 33 zenye thamani ya mamilioni ya fedha) tumboni.

Marehemu alikutwa na hati ya dharura ya kusafiria nchi za nje ambayo haikuonyesha anakoelekea.Wanawake wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na maiti iliyokuwa na dawa za kulevya tumboni.

Friday, September 20, 2013

HATARI:DAWA ZA KULEVYA SASA KUCHANGANYWA NA SUMU YA PANYA


Dawa mpya ya Kulevya inaitengesha jamii nchini humo.
Nyaope ni dawa ya kulevya yenye mchanganyiko wa vitu vingi, na bei yake haifikii hata Dola Mbili na Nusu, lakini inaathiri maisha ya vijana wengi.
Uhalifu unaohusihwa na dawa za Kulevya unaongezeka Afrika Kuisni. Watu wameitaka serikali kushughulikia vyema suala hili. Suluma Kassim anasimulia
TAZAMA VIDEO HAPA

Wednesday, September 18, 2013

WALIOLIPUA MABOMU KWENYE MKUTANO WA CHADEMA JIJINI ARUSHA WAKAMATWA...!!


 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo. 

WATUHUMIWA walioingiza mabomu ya kurushwa kwa mkono yaliyotupwa Arusha Mei na Juni katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti na kwenyemkutano wa wa hadhara wa Chadema, Soweto mkoani Arusha, wamekamatwa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alisema hayo jana katika mkutano wa siku moja wa kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha, uliofanyika eneo la Olasiti.
“Watuhumiwa hawa siku si nyingi Kamanda wa Polisi wa Arusha, ataweka majina hadharani, watu wawajue na si wageni, ila kwa sasa kinachochunguzwa ni kutaka kufahamu waliowatuma kuingiza mabomu hayo na kwa lengo gani."
Mulongo alisema kwa sasa Polisi iko katika hatua za mwisho za mahojiano na watuhumiwa hao, ambapo mbali na kutaka kufahamu waliowatuma na malengo yao, pia wanatarajia kupata taarifa za waliorusha mabomu hayo.
Malengo mengine kwa mujibu wa Mulongo ni kuwafahamu watu wote waliopewa zabuni ya kuingiza mabomu hayo, ili hatua za kisheria zifuate.
Mulongo aliomba wananchi waendelee kutulia wakisubiri matokeo ya Serikali na hata wakitajwa wahusika waiachie Polisi ifanye kazi yake. Mabomu hayo yalirushwa Mei 5 kanisani Olasiti na Juni 15 uwanja wa Soweto, wakati wa hitimisho la kampeni za udiwani za Chadema mkoani hapa.

Tuesday, September 17, 2013

Polisi wawili wakamatwa na risasi 3,000




Mara. Polisi wawili wa Musoma, Mkoa wa Mara na Kibaha, Pwani wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha risasi 3,000 kutoka Musoma kwenda Dar es Salaam.
Wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo ni aliyekuwa mtunza chumba cha silaha Kikosi cha FFU Musoma na mwenzake mwenye cheo cha Koplo Wilaya ya Kibaha, Pwani. Inadaiwa walikamatwa Juni 2, mwaka huu saa 11:00 alfajiri.
Watuhumiwa wanashikiliwa Kituo cha Polisi Musoma na wamefunguliwa jalada MUS/RB/2465/013 wizi wa risasi 1,056, wanasubiri taratibu zingine za polisi.

Monday, September 16, 2013

Baada ya kumwaga Damu zaidi ya miaka 20, Somalia yakubali kukaa mezani,kujadili tofauti zao.

Mkutano kuhusu Somalia Brussels

EU kwa ushirikiano na serikali ya Somalia, Iimeandaa kongamano la kimataifa Brussels kutathmini hali maendeleo nchini Somalia dakika 45 zilizopita

http://www.bbc.co.uk/swahili/
Somalia imeshuhudia maendeleo si haba tangu Al Shabaab kufurushwa mjini Mogadishu.
Muungano wa Ulaya kwa ushirikiano na serikali ya Somalia, hii leo umeandaa kongamano la kimataifa mjini Brussels kutathmini hali inavyoendelea nchini Somalia
Wanadiplomasia wanasema wanatarajia kuwa wahisani wataahidi kuchangisha mamilioni ya dola kama msaada kwa Somalia kwenye mkutano huo.