- WATUMISHI WOTE SASA KUHAKIKIWA VYETI VYAO
- ASKARI WALIOVITUMIA KUPANDA VYEO KUKIONA
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, limetoa mwezi mmoja kwa watumishi wake wote kuwasilisha vyeti vyao ili viweze kufanyiwa
uhakiki ili kubaini kama kuna vyeti feki.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Job Masima, aliyasema hayo Dar es
Salaam jana wakati wa Mafunzo ya Elimu ya Hifadhi ya
Jamii yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya
Jamii (SSRA).
Alisema kuanzia leo,
watumishi wote waliopo chini ya Wizara hiyo watapaswa kuwasilisha vyeti vya
vyuo walivyosomea."Natoa mwezi mmoja kuanzia leo hadi Januari, wawasilishe
yeti vyao wizarani viweze kukaguliwa...baada ya ukaguzi tutafuatilia maeneo
waliyosomea ili kubaini kama kuna askari wanaotumia vyeti
feki," alisema.





